latest Post

MITISHAMBA SABA MUHIMU NA FAIDA ZAKE MWILINI


Mitishamba ni mimea ambayo huwa tunakutana nayo katika maisha yetu ya kila siku, na pia huwa tukiitumia katika vykula vyetu na hata katika shughuli kadha wa kadha za jadi. Katika karne hii ya sayansi na teknolojia madaktari mbalimbali duniani wamejitahidi kutengeneza madawa ya kutibu,  kukinga mwili na magonjwa pia kutengeneza madawa ya kuuwa wadudu waaribifu kama vile mende na hata mbuu. 
Ni kweli kwamba watu wengi hutumia mitishamba kwa matumizi yao ya kawaida bila kujua matumizi na kazi sahihi ya mitishamba hiyo katika miili yao, hivyo kutofanya matumizi stahiki.
Mitishamba inayofahamika katika jamii zetu na faida zake ni kama vile
  • Kitunguu saumu
Kitunguu saumu ni moja wapo ya mitishamba tunayoitumia katika vyakula vyetu vya kila siku bali watumiaji wengi hutumia vitungu hivyo bila kujua faida zake. Vitunguu saumu vina viuavijasumu(antibiotics) ambavyo husaidia kulinda mwili na magonjwa ya sababishwayo na bacteria, na pia husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata magonjwa kama vile shinikizo la damu au magonjwa ya moyo. kwa watu wanaopenda kupungua ni dhahiri ya kwamba vitunguu saumu ni msaada mkubwa kwa kigezo cha kuweza kuondoa mafuta mwilini (cholesterol). Hivyo inashauriwa mtu kutumia vitunguu saumu angalau mara tatu kwa wiki.



  • Tangawizi
Tangawizi ni aina moja wapo ya mitishamba yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu, na hutumika katika maisha yetu ya kila siku. Tangawizi husaidia kutibu tatizo la tumbo la kuhara, husaidia kukabiliana na kansa ya utumbo mkubwa na pia husaidia kukabiliana na kikohozi kikali . Kwa kipindi cha awali kabla ya ugunduzi wa dawa za kisasa nchi za ukanda wa joto walikuwa wanatumia Tangawizi ili kutibu majeraha ya moto kwa kusaga na kuchanganya na maji na kumwagia pahali palipo athiriwa ilikupunguza maumivu makali.

  • Almond
Almond yasifika kwa upatikanaji wa mafuta yenye virutubisho kama vile magnesium, calcium, proteins, phosphorus na riboflavin. kutokana na hayo Almond hutumika kukabiliana na magonjwa kama vile Alzheimer's(upungufu wa kumbukumbu uzeeni), magonjwa ya moyo, magonjwa ya ngozi na pia Almond hutumika kuimarisha mifupa na meno na zaidi ni  kupunguza mafuta ya mwili(cholesterol). Wataalam wa lishe wanapendekeza watu watumie Almond kwenye vyakula vyao zaidi ili kupunguza kasi ya mwili kuzeeka na kuwa na afya njema.





  • Mint 
Mint ni moja wapo ya mitishamba ambayo inasifika kwa kutibu matatizo ya ngozi kama vile chunusi, pia hutibu asthma kwakulifanya koo huru kwa kupitisha hewa na hata kupunguza maumivu ya kichwa .Utafiti unaonyesha ya kwamba asilimia kubwa ya watu wanao tumia mitishamba hii huwa wanakumbukumbu sana kulingana na utafiti uliofanya kwenye bara la Asia. Matumizi ya mint yaweza kuwa kwa kutafuna mmea wake pekee na hata kwa kuchanganya kwenye chakula cha kawaida.

  • Mchaichai
Mchaichai ni mmea ulio jaliwa virutubisho kama vile magnesium, vitamini A&C, potassium na madini ya chuma, vyote hivyo hujenga na kuimarisha mwili. Mchachai hurutubisha ngozi, hutumika kutoa sumu mwilini, hutumika kuondoa flu na pia hutumika kukabiliana na gonjwa la cancer ya tumbo na uzazi. Maandalizi ya mchaichai kwa mara nyingi ni kwa kuchemsha maji na mmea huo ili kutengeneza chai.

  • Aloe_vera
Aloe vera ni aina ya mitishamba inayofahamika na wengi ulimwenguni na wengi hutumia kwa matumizi mbali mbali kama vile kutengeneza sabuni, shampoo na hata madawa. Kutokana na virutubisho vyake kama vile vitamini, madini na amino acid  aloe vera hutumika kuhimarisha ngozi, kuongeza kinga ya mwili, kuhimarisha nywele, kuondoa sumu mwilini na pia kupunguza unene. Madaktari wengi wanashauri ya kwamba watu watumie bidha za aloe vera  zaidi ili kujihakikishia afya bora

  • Gotu_kola
Gotu kola ni aina ya miti shamba ipatikanayo sehemu yenye vyanzo vya maji kama mito,maziwa na hata bahari. Gotu kola hutumiwa kutengeneza salad, supu na hata vinywaji asilia, mmea huu unafahida mbali mbali kwenye mwili wa binadamu kama vile kutibu majeraha ya mwili, husaidia kupunguza maumivu ya vidonda vya tumboo(ulcers), huondoa sumu mwilini na pia hutumika kuhakikisha kuwa presha ya damu mwilini ipo katika hali ya usawa.


Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali na maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255653009477
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit),
 twitter-(kuafit) 







About Kuafit

Kuafit
Recommended Posts × +

0 comments:

KUPUNGUZA UZITO KWA MAJI YA BARIDI

Watu wengi katika jamii hupendelea kuoga na maji ya moto katika majira yote ya hewa lakini kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi kam...