latest Post

MAMBO 6 MUHIMU YA KUZINGATIA KWA MTU MWENYE KISUKARI WAKATI WA MAZOEZI

 

 Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kupata tatizo la kongosho kushindwa kutengeneza homoni ya insulin hivyo kushindwa kubadili glukosi ya mwili ili kutengeneza nguvu. Watu wenye ugonjwa huo wa kisukari hua wanahatari ya kusumbuliwa na maradhi mengine kama vile maradhi ya moyo,tatizo la kutokuona,mshtuko wa mwili.
 Ugonjwa wa kisukari upo katika namna mbili, ya kwanza ni aina ya kwanza(type 1) na aina ya pili(type 2). Aina ya kwanza(type 1) ya kisukari hutokea endapo mtu  atashindwa kutengeneza homoni ya insulin ya kutosheleza mahitaji ya mwili. Aina ya pili (type 2) hutokea endapo mtu atakapo shindwa kuitumia homini ya insulin kikamilifu hatakama itakuwa imezalishwa ya kutosheleza mwili.
     Madaktari huwa wanashahuri sana kuwa watu wenye kisukari wafanye mazoezi ili kuwezesha afya zao kuwa katika hali nzuri, hivyo wengi hujitaidi kujiunga na gym ilikupata mwongozo mzuri wa ufanyaji wa mazoezi. Kutokana na wingi wa watu wenye ugonjwa wa kisukari kufanya mazoezi na pia kujiunga na gym basi ni vyema watu hao wajue mambo 6 muhimu ya kuzingatia kabla ya kujiunga na gym ama kuanza mazoezi.
  1. Pata ruhusa ya daktari na kuwa mwangalifu wa kiasi cha glukosi mwilini.
  Inashahuriwa kwamba ni vyema kupata ruhusa ya daktari kwanza kabla ya kujiunga na gym ama kuaza mazoezi, maana yaweza kuwa afya yako ni dhohofu na kusababisha matatizo mengine. Mtu mwenye kisukari anapaswa kuwa makini na kiwango cha glukosi mwilini ambapo hupimwa na kifaa kitwacho blood sugar glucose meter(BSGM). Inashahuriwa kwamba mtu akipima na akikuta kiwango cha glukosi mwilini ni zaidi ya 250mg/dl basi itabidi ajihadhari na mazoezi magumu na ikiwa kiwango kitakuwa zaidi ya 300mg/dl basi mtu huyo awemwangalifu zaidi katika mazoezi afanyayo.


     2. Linda miguu mbali na sugu na majeraha yanayowekutokana na misuguano 

  Uwangalifu wa miguu unahitajika sana kwa watu wenye kisukari, na hasa kwa mazoezi kama kukimbia,aerobics, na hata kuruka kamba. Inashahuriwa kwamba mtu mwenye ugonjwa wa kisukari awe  anapaka mafuta ya silica gel na pia kuvaa soksi za polyster ama blend cotton polyster. Kwa kufanya hayo inamwezesha mtu kubaki mnyevu miguuni na pia kupunguza uwezekano wa madonda yatokanayo na sugu za miguu.   3. Fanya mazoezi ya kuchangamsha na kupasha mwili kabla ya zoezi lenyewe .

    Mtu mwenye kisukari anashahuriwa kuanza na mazoezi ya kuapasha viungo vya mwiili kama vile kutembea na kuendesha baiskeli kwa mda wa dakika 5 mpaka 10 kabla ya zoezi lenyewe. Kwa kufanya mazoezi hayo kunasaidia kutayarisha misuli ya mwili, mapafu, moyo na hata miguu kuweza kustahimili mazoezi mengine endelevu baada ya hapo.  4. Fanya mazoezi kulingana na aina ya kisukari na pia umri wako.

    Kutokana na jarida la Diabetese core 13(Technical review) inasemekana kwamba mtu mwenye aina ya kwanza ya kisukari(type 1) ana uwezo wa kufanya mazoezi mengi kuliko mtu mwenye aina ya pili ya kisukari(type 2). Inashahuriwa ya kwamba kwa watu wenye kisukari mazoezi ya kutumia uzito  mkubwa na mazoezi magumu yafanywe na watu wenye umri chini ya miaka 35, na kwa wale wenye miaka juu ya 35 wafanye mazoezi yenye kutumia uzito mdogo ama wastani. Kwa wale wenye umri juu ya 35 wanaweza kutumia uzito mdogo kwa kurudia mara nyingi iwezekanayo ili kujenga nguvu ya misuli.


  5. Zingatia unywaji wa maji
   
   Maji ni kitu muhimu sana mwilini maana huchangia asilimia kubwa wa ufanisi wa vyungo vingine vya mwili. Kwa mtu mwenye kisukari anashahuriwa kunywa lita 2 na zaidi ya maji kwa siku na pia kunywa maji kabla ya mazoezi. Kwa kuto kunywa maji kunaweza kusababisha moyo kutokufanya kazi kwa ufanisi, na hata pia kwa kutokunywa maji yaweza kuadhiri kiwango cha glukosi mwilini.


 6. Jua na zingatia vyakula vinavyo kupasa kula

  Mtu mwenye kisukari anashahuriwa kuwa apunguze ulaji wa  vyakula vya wanga kwa kiasi kikubwa na hata pia vyakula vyenye mafuta sana vinapaswa kupunguzwa. mwanamazoezi anyeuguwa ugonjwa wa kisukari anashahuriwa kula vyakula vyenye protini ya wastani kama nyama ya kuku, samaki na nyama nyekundu kwa kiasi kidogo pia anaweza kula  mboga na matunda kwa sana ili kuweza kumpatia nguvu kama chanzo cha glukosi asilia.

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali au maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255653009477
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit),

 twitter-(kuafit) 

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...