latest Post

VYAKULA VYINAVYO SAIDIA KUPUNGUZA UNENE


Kupunguza mwili mara nyingi huwa ni kazi ngumu yenye kuhitaji jitihada binafsi ili kuweza kufanikisha lengo, bali jitihada kidogo yaweza kutosheleza endapo mtu akijua jambo gani linalomhitaji afanye ili aweze kutimiza lengo. 

Katika mambo makuu ya kuzingatia katika swala kuu la kupunguza mwili ni vyakula, mazoezi na nidhamu binafsi. Mara nyingi watu hufeli kwenye swala kubwa la vyakula, na kikubwa kinachowakwamisha watu ni kwenye kujua ni chakula gani kula ili kuweza kupunguwa.
Vyakula vya kupunguza mwili vipo vingi bali kuna vile vyenye kuleta matokeo mapema zaidi ya vingine na  ni kama vile-


  • Mboga za majani
Ukitoa mbali kwamba mboga za majani kuwa na kiwango kikubwa cha vitamini A, mboga hizo zinasemekana kuwa na kiwango kidogo cha calorie(6) na huwa ni pendekezo sahihi kwa mtu anayetaka kupungua. Mtu anashauriwa kutumia mboga za majani zaidi kwenye chakula chake cha kila siku ili kuweza kupata matokeo kwa haraka  • Maharage
Utafiti naseme ya kwamba maharage yanasaidia mtu kuweza kutengeneza homoni ya cholecystokenin kwa wingi zaidi mwilini. homoni hiyo humsaidia mtu kuweza kuhifadhi chakula kwenye tumbo kwa kiasi kikubwa. Kutokana na hayo basi mtu anayetaka kupunguza mwili anaweza kukaa mda mrefu bila ya kula hovyo na asisikie njaa

  • Green tea
 Utafiti unaonyesha yakwamba green tea husaidi sana kupunguza mwili kutokana na uwepo wa catechins kwa wingi ambayo ni kemikali inayosaidia kuchoma mafuta mwili yasiyo hitajika na mwili. Inashahuriwa yakwamba ni vyema kunywa chai hii mara mbili kwa siku kwa watu wanaotaka kupunguwa.


  • Peaz
Mapeaz ni mojo wapo ya matunda yenye kusadikika kuwa na kiwango kikubwa cha petcin fiber ambacho humsaidia mtu kukaa mda mrefu bila ya kuhitaji kula. Mtu anayetamani kula anashahuriwa kula tunda hili hasa kama sehemu ya lishe yake, kwa kufanya hivyo humsaidia mtu kutokutamani kula mara kwa mara.


  • Mchele wa kahawia
Utafiti unaonyesha kuwa kikombe kimoja cha mchele wa kahawia huwa na kiwango cha mpaka  1.7 gram ya kemikali ya kupunguza wanga(starch) zaidi ya mchele mweupe. Mchele wa kawahia pia husifika kwa kuwa na calorie kihasi kidogo na hushibisha sana hivyo hupendekezwa kama moja wapo ya chakula cha kupunguza mwili. 


  • Almond
Utafiti wa kisayansi unaonyesha yakwamba mbegu za almond zina kiwango kidogo cha calorie, na pia mbegu hizi zimebarikiwa na mafuta yenye manufaa kwenye mwili. Watu wenye kutumia mbegu za almond wanasemekana wanauwezekano mkubwa sana kupungua zaidi kuliko mtu anayetumia lishe ya kawaida.
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali na maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa kusoma andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako  kwenye linki ya SUBSCRIBE.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255653009477
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit),
 twitter-(kuafit) 
About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...