latest Post

UMUHIMU NA FAIDA YA KUFANYA MAZOEZI


Kulingana na dunia ya sasa ambayo imewalazimu watu kuendana na utandawazi imewafanya watu kubadili mifumo ya maisha inayotufanya kutotulazimu kutumia nguvu nyingi kufanya kazi na pia vyakula vingi vinatengenezwa kwenye viwanda kwa kemikali.
Kuna umuhimu mkubwa sana unaoletwa na ufanyaji wa mazoezi kwa watu wote bila kujali jinsia wala rika, kufanya mazoezi kunafaida nyingi kubwa kiafya kwa dunia ya sasa kama vile;


  • Hupunguza uwezekano wa kupata gonjwa la presha
Chanzo kikubwa cha presha ni mafuta yanayoziba njia(mishipa) ya damu ambapo kunafanya mzunguko wa damu kuwa mgumu na hivyo kusababisha presha . Kwa kufanya mazoezi kunafanya njia za damu kuzibuka na pia kufanya mtu kuwa na mapigo ya moyo makubwa ambapo husaidia mzunguko wa damu kuwa mzuri.

  • Husaidia kupunguza uzito wa mwili
Uzito wa mwili unaotokana na kula chakula cha wanga na mafuta unaweza kupunguzwa kwa kufanya mazoezi mara kwa mara. kutokanan na utafiti uliofanywa na wanasayansi ni kwamba kadiri ya mtu anavyofanya mazoezi ndivyo mtu anavyo choma mafuta ya mwili na ndivyo anavyoweza kupunguza calorie zilizozidi ndani ya mwili

  • Huongeza na kuimarisha misuli ya mwili

Misuli huimarika zaidi kwa kufanya mazoezi hasa mazoezi yanayo muhitaji mtu kutumia nguvu nyingi. Mazoezi kama vile kunyanyua vitu vizito kama vile vyuma na mazoezi ya vyungo yanayo muhitaji mtu kubeba uzito wa mwili wake hujenga haraka misuli ya mwili na kumpa mtu muonekano mzuri.

  • Huondo uwezekano wa mtu kupata kisukari
Mazoezi yaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha mtu kukabiliana  na kisukari cha aina ya pili(melitus), kwa kufanya mazoezi kunamhahikishia mtu kuwa glucose(sukari) iliyopo kwenye mwili intumika ipasavyo.
Hivyo mazoezi ni chanzo kikubwa cha mwili kuweza kumeng'enya glucose na kupunguza uwezekano wa ugonjwa wa kisukari

    • Huongeza hamu ya tendo la ndoa
Kwa kufanya mazoezi tezi(gland) ya endocrine inalazimika kutoa homoni nyingi za mwili zinazohitajika. Moja wapo ya homoni inayotolewa kwa wingi kwa mtu anyafanya mazoezi ni androgen ambayo inahitajika sana na jinsia zote mbili kusaidia mtu kuwa na mihamko ya kimapenzi na husaidia ufanisi kwa kuhimarisha maungo ya siri.


  • Huongeza furaha kwa kupunguza msongo wa mawazo
Mtu anyaefanya mazoezi ni rahisi sana kuwa mtu mwenye furaha wakati wote maana akili yake ni ngumu sana kuwa na msongo wa mawazo maana kwa kufanya mazoezi kuna mfanya ajifunze kujipenda yeye na mwili wake hivyo sikolojia ya mtu huwa chanya wakati wote.

  • Huongeza kumbukumbu
Utafiti unaonyesha kuwa mtu anyefanya mazoezi huchangia kuhimarisha mishipa ya fahamu kwa kiasi kikubwa sana, pia uathiri sehemu ya ubongo itwayo hippocampus ambayo uhusiana na kumbukumbu na kuifanya kuwa changamfu na hivyo kuimarisha kumbukumbu kwa mtu. 

  • Uhimarisha afya 
Kwa kufanya mazoezi ina hakikishia mwili kuwa na afya kwa kuongeza seli za ulinzi mwilini. Hivyo basi kwa kuongeza seli za ulinzi inakuwa ngumu kwa mtu kupata maradhi hovyo ama kuuugua magonjwa madogodogo maana ulinzi wa mwili ni mkubwa. Inashauriwa sana na madaktari kuwa watu wanapaswa kufanya mazoezi ilikupata afya bora.
Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali na maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa andiko jengine kama hili basi jisajili kwa kuweka anuani yako juu kwenye linki ya KUJISAJILI.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255653009477
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit),
 twitter-(kuafit) 

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...