latest Post

FAIDA ZA KIAFYA NA UMUHIMU WA TIKITIMAJI


Tikiti maji ni tunda linalotambulika na watu wengi duniani kutokana na upatikanaji wake umekuwa mkubwa, inasadikika kuwa tunda hili liligundulika kwa mara ya kwanza maeneo ya jangwa la kalahari. Tunda la Tikiti ni tunda moja wapo lenye faida kubwa  kwenye mwili, umuhimu na faida zenyewe ni kama zifwatazo


  • Huongeza kiasi cha maji mwilini
Utafiti unonyesha kuwa tunda la tikiti maji limejengwa kwa asilimia takribani tisini (90%) na maji na hivyo mtu atakaye fanikiwa kulila atakuwa amejiongezea kiasi kikubwa cha maji mwilini bila kusahau kiasi kikubwa cha fiber.

  • Huboresha hali ya Moyo kiafya
Tikiti limebarikiwa na acid kama amino acid yenye kusaidia utanukaji wa mishipa ya damu na hivyo upitishaji mzuri wa damu, pia tikiti huwa na kemikali itwayo lycopene yenye kusaidia kupunguza mafuta(cholestrol) yanayoweza ziba njia ya damu.

  • Huimarisha ngozi na nywele
Mbali na tikiti kuwa na lycopene na carotene inayo saidia kwenye utengenezaji na seli za ngozi pia tikiti limebarikiwa na vitamini A ambayo husaidia kuhimarisha nywele na ngozi zililizo kauka, bila ya kusahau vitamini C inayo saidia kuimarisha ngozi na kufanya nywele kuwa ngumu na himara.

  • Huongeza nguvu za kiume
Citrulline iliyopo kwenye tikiti ikibadilishwa kuwa argenine mwilini inakuwa ni amino acid yenye kusaidia utanukaji wa njia za damu na hivyo kusaidia damu nyingi kulekea kwaenye sehemu za siri na hivyo kurutubisha na pia kuimarisha sehemu hizo. Inasemekana tikiti hutumika kutengezea viagra asili kwa sababu hiyo.

  • Hushusha presha ya damu
Presha ni sababu kubwa ya mtu kupata mshtuko wa moyo na pia mstuko wa mlili(stroke) na tikiti husaidia kupunguza presha kutokana na uwepo wa citrulline.

  • Kutibu matatizo ya Figo
Tikiti ni muhimu kwa kutibu na kuimarisha figo maana limebarikiwa na calcium na potassium ambapo husaidia kutoa nje sumu zote zilizo kwenye figo, pia hupunguza kiasi cha acid kweye figo hivyo kupunguza  uwezekano wa kupata magonjwa ya figo.

  • Hupunguza uwezekano wa kupata cancer
kutokana na uyatikanaji wa lycopene kwenye tunda la tikiti imekuwarahisi kukabiliana na cell za cancer kutokanan na lycopene hupunguza uzalishaji wa insulin ambayo ni chanzo cha kupunguza uwezekano wa kupata na pia kusambaa kwa cancer mwilini  

Kama umeipenda andiko hili basi gonga NZURI  na  kwa maswali na maoni zaidi basi tuandikie baada ya andiko hili, na pia kama ungependa maandiko mengine kama haya basi jisajili kwa kuweka anuani yako juu kwenye linki ya KUJISAJILI.
Pia waweza tuandikia kwa email yetu Kuafit08@gmail.com
Kwa number yetu ya Tigo +255653009477
Instagram account yetu  (KUAFITI), Facebook-(kuafit),
 twitter-(kuafit) 

About benson godfrey

benson godfrey
Recommended Posts × +

DIET YA KUTOA SUMU MWILINI NA KUPUNGUZA UNENE KWA HARAKA

Habari zenu wadau wa KUAFIT! leo tutaongelea kuhusiana na elimu ya lishe ambayo itahusiana na diet ambapo tutaelezea mambo mengi san...